Media Centre
Press Release
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga kwa niaba ya watoa mada kuu walioshiriki katika Kongamano la Nne la Kitaaluma la Biashara na Uchumi lililofanyika jana jijini Dodoma chini ya uratibu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Dkt. Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alikabidhi vyeti kwa kutambua mchango wa wazungumzaji hao kwenye tasnia ya Taaluma, Biashara na Uchumi na kipekee, aliishukuru Tume ya Tehama kwa kutekeleza vyema majukumu yake tangu ilipoasisiwa katika Serikali ya Awamu ya Nne. (Mpiga Picha Wetu).
TUME ya Tehama nchini (ICTC) na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) zimesaini Mkataba wa Maelewano (MoU) kwa ajili ya kujenga Maabara ya Kutengeneza, Kukarabati na
Kuunganisha Vifaa vya Kieletroniki nchini.
Maabara hiyo ya kisasa ambayo inatarajiwa kujengwa na tume ndani ya shirika hilo inatarajiwa kuwa fursa kubwa kwa vijana kustawisha bunifu zao nchini.
Pia, taasisi hizo za umma zitashirikiana katika sekta zingine kama kuunganisha vifaa vya kielektoniki, kufanya matengezo vifaa vilivyoharibika. Vile vile kutoa mafunzo ya kitalam kwa wataalam wa TEHAMA na kuhuisha vifaa vilivyokwisha muda wake ili viweze kuingia sokoni tena kwa matumizi.
DAR-Tume ya TEHAMA nchini imesema kuwa, inashirikiana na Rais na Mkuu wa Chuo cha Turku,Prof.Vesa Pekka Taatila kutoka nchini Finland ili kuleta intaneti mpya inayotumia mikono zaidi kutengeneza mano wa kitu halisi kwenye kompyuta na kuunganisha moja kwa moja kwenye matumizi
ijulikanayo kama Metaverse.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi leo Agosti 7, 2024 ametembelea ofisi za Tume ya TEHAMA (ICTC) ambapo pamoja na kupitishwa kwenye majukumu yanayotekelezwa na Tume hiyo pia ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ubunifu cha TEHAMA kilichopo Upanga Jijini Dar es Salaam